Sataranji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Chess)
Ubao wa chesi kabla ya kuanza mchezo; saa zatumiwa wakati wa mashindano anbapo kila mchezaji anapewa muda fulani tu.

Sataranji (kutoka Kiajemi/Kiarabu شطرنج shatranj; pia: chesi kutoka Kiingereza chess) ni mchezo wa ubao kwa wachezaji wawili.

Ubao wa sataranji

Ubao wa sataranji huwa na umbo la mraba na ndani yake kuna miraba midogo 64 inayobadilishana kwa rangi nyeupe na nyeusi. Kuna pia badiliko la rangi za kahawia nyeupe na kahawia nyeusi au rangi mbalimbali.

Kete za sataranji

Jina la kete Herufi ya kifupi[1] Picha
Shaha, kete kuu
K (King)
ShahaShaha
Malkia
Q (Queen)
MalkiaMalkia
Ngome
R (Rook)
NgomeNgome
Sataranja
B (Bishop)
SataranjaSataranja
Farasi
N (Knight)
FarasiFarasi
Kitunda
P (Pawn)
KitundaKitunda

Kila mchezaji huwa na kete 16 zinazopangwa kwa namna maalumu ambayo ni sawa kwa kila upande na kila safari. Isipokuwa zinatofautiana kwa rangi, kwa hiyo kuna mchezaji mweupe na mchezaji mweusi. Mweupe huanza mchezo; safari inayofuata wachezaji wanabadilishana rangi.

Kete ni za aina mbili:

  • vitunda vinane ambavyo ni kete zenye nguvu ndogo zinasimamishwa kwenye mstari wa pili mbele ya mchezaji. Vitunda vyote ni sawa, hakuna tofauti kati ya kitunda na kitunda.
  • kete 8 za juu ambazo ni ngome 2, farasi 2, sataranja 2, malkia 1 na mfalme 1.

Kete za juu zinapangwa kwa namna ifuatayo: ngome -farasi -sataranja -malkia -shaha -sataranja -farasi -ngome.

Mchezo

Mchezo huanzishwa na mchezaji mwenye kete nyeupe anayehamisha kete ya kwanza jinsi anavyoamua. Halafu zamu ya mwenye kete nyeusi hufuata na mchezo unaendelea kwa zamu.

Kila kete ina mwendo wake wa pekee. Kete haiwezi kuhamia mraba wenye kete ya rangi yake. Lakini ikimaliza mwendo wake kwenye mraba wenye kete ya rangi nyingine inaikamata maana yake kuiondoa kutoka ubaoni na kuchukua nafasi yake kwenye mraba. Kete iliyokamatwa hairudi tena: ni kama imefungwa au kufa.

Katika mwendo wake kete haiwezi kupita juu ya miraba yenye kete nyingine isipokuwa kete ya farasi ambayo ina uwezo wa kuruka. Vinginevyo mwendo ama unakwisha mbele ya kete nyingine au inaweza kuikamata na kuchukua nafasi yake.

Mwisho: Shaha nyeusi ameshindwa; hana mahali anapoweza kwenda bila kutishiwa tena.

Shabaha ya mchezo ni ushindi. Ushindi unapatikana kama kete ya shaha inatishwa moja kwa moja na kete nyingine ilhali haina nafasi ya kuhamia mahali pasipo tishio. Shaha haiwezi kukamatwa; ikiweza kushambuliwa bila mahali pa kukimbilia, mchezo unakwisha. Hali hii huitwa kwa lugha nyingi "mat" ambalo ni neno la Kiajemi linalomaanisha "amekwisha, hawezi". Kwa Kiingereza ni "checkmate".

Mwendo

Kuanzia upande wa kushoto hapo kuna shaha mweupe, ngome nyeusi, malkia mweusi, kitunda cheupe, farasi nyeusi na sataranja nyeupe.

Shaha Shaha ni kete kuu katika mchezo; inatembea hatua 1 (=mraba 1) kila upande. Kuna hatua ya pekee ambayo ni kuruka ngome.

Malkia

Ngome

Sataranja

Farasi

Kitunda
Kete ya Kitunda hutembea mbele bila kunyoka tu hadi mwisho wa ubao. Mwendo wake ni hatua ya mraba mmoja. Lakini hatua yake ya kwanza kama haijatembea bado ina nafasi ya kutembea hatua mbili za mraba. Mara nyingi mchezaji mwenye kete nyeupe huanza mchezo kwa kusukuma kitunda kilichopo mbele ya shaha.

Kitunda kikitembea mbele hakina uwezo wa kukamata kete ya adui iliyopo mbele yake. Kituda hukamata kete iliyopo upande wa kushoto au kulia wa mraba mbele yake.

Kama kitunda kinafikia mstari wa mwisho wa ubao kinaondolewa na kubadilishwa kwa kete nyingine yoyote isipokuwa kete kuu ya shaha. Badiliko la kitunda huwa ni uamuzi wa mchezaji wake.

Sataranji ya posta

Ni aina ya chess ambapo wapinzani huwasilisha mienendo yao kwa kila mmoja kupitia kadi za posta. Hivi sasa barua pepe inatumika. Muda wa mabadiliko unakadiriwa kwa siku na mchezo unaweza kuchukua miezi au miaka kukamilika.

Shirikisko la kimataifa la Mawasiliano la Chess (ICCF) [2] lililoanzishwa mwaka wa 1951, lina jukumu la kuandaa Olimpiki yake na Mashindano ya Dunia.

Mashindano ya Dunia ya ICCF

# Miaka Bingwa Utaifa
1 1950-1953 Cecil Purdy Bendera ya Australia Australia [3]
2 1956-1959 Viacheslav Ragozin Bendera ya Urusi Urusi [4]
3 1959-1962 Alberic O'Kelly Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji [5]
4 1962-1965 Vladimir Zagorovsky Bendera ya Urusi Urusi [6]
5 1965-1968 Hans Berliner Marekani [7]
6 1968-1971 Horst Rittner Bendera ya Ujerumani Ujerumani [8]
7 1972-1976 Jakob Estrin Bendera ya Urusi Urusi [9]
8 1975-1980 Jorn Sloth Bendera ya Denmark Denmark [10]
9 1977-1983 Tonu Oim Estonia [11]
10 1978-1984 Vytas Palciauskas Marekani [12]
11 1983-1989 Fritz Baumbach Bendera ya Ujerumani Ujerumani [13]
12 1984-1991 Grigory Sanakoev Bendera ya Urusi Urusi [14]
13 1989-1998 Mikhail Umansky Bendera ya Urusi Urusi [15]
14 1994-2000 Tomu Oim Estonia [16]
15 1996-2002 Gert Timmerman Bendera ya Uholanzi Uholanzi [17]
16 1999-2004 Tunc Hamarat Austria [18]
17 2002-2007 Ivar Bern Norway [19]
18 2003-2005 Joop van Oosterom Bendera ya Uholanzi Uholanzi [20]
19 2004-2007 Christophe Leotard Bendera ya Ufaransa Ufaransa [21]
20 2004-2011 Pertti Lehikoinen Bendera ya Ufini Finland [22]
21 2005-2008 Joop van Oosterom Bendera ya Uholanzi Uholanzi [23]
22 2007-2010 Aleksandr Dronov Bendera ya Urusi Urusi [24]
23 2007-2010 Ulrich Stephan Bendera ya Ujerumani Ujerumani [25]
24 2009-2011 Marjan Semri Slovenia [26]
25 2009-2013 Fabio Finocchiaro Bendera ya Italia Italy [27]
26 2010-2014 Ron Langeveld Bendera ya Uholanzi Uholanzi [28]
27 2011-2014 Aleksandr Dronov Bendera ya Urusi Urusi [29]
28 2013-2016 Leonardo Ljubicic Kroatia [30]
29 2015-2018 Aleksandr Dronov Bendera ya Urusi Urusi [31]
30 2017-2019 Andrey Kochemasov Bendera ya Urusi Urusi [32]
31 2019-2022 Fabian Stanach
Christian Muck
Ron Langeveld
Bendera ya Poland Poland
Austria
Bendera ya Uholanzi Uholanzi
[33]
32 2020-2022 Jon Edwards Marekani [34]


Michezo ya Olimpiki ya ICCF

# Miaka Medali ya dhahabu Medali ya fedha Medali ya shaba
01. 1949-1952 Hungaria Chekoslovakia Bendera ya Uswidi Uswidi
02. 1952-1955 Chekoslovakia Bendera ya Uswidi Uswidi Bendera ya Ujerumani Ujerumani
03. 1958-1961 Muungano ya Sovieti Hungaria Yugoslavia
04. 1962-1964 Muungano wa Sovieti Ujerrumani ya Kidemokrasia Bendera ya Uswidi Uswidi
05. 1965-1968 Chekoslovakia Muungano wa Sovieti Ujermani Magharibi
06. 1968-1972 Muunganowa Sovieti Chekoslovakia Ujerumani ya Kidemokrasia
07. 1972-1976 Muungano wa Sovieti Bulgaria Uingereza
08. 1977-1982 Muungano wa Sovieti Hungaria Uingereza
09. 1982-1987 Uingeresa Ujerumani Magharibi muungano wa Sovieti
10. 1987-1995 Muungano wa Sovieti Uingereza Ujerumani ya kidemokrasia
11. 1992-1999 Chekoslovakia
Bendera ya Ujerumani Ujerumani
Bendera ya Kanada Kanada
Scotland
12. 1998-2004 Bendera ya Ujerumani Ujerumani Lithuania Latvia
13. 2004-2009 Bendera ya Ujerumani Ujerumani Bendera ya Ucheki Czech Republic Bendera ya Poland Poland
14. 2002-2006 Bendera ya Ujerumani Ujerumani Lithuania Marekani
15. 2006-2009 Norway Bendera ya Ujerumani Ujerumani Bendera ya Uholanzi Uholanzi
16. 2010-2016 Bendera ya Ucheki Czech Republic Bendera ya Ujerumani Ujerumani Bendera ya Ufaransa Ufaransa
19050 17. 2009-2012 Bendera ya Ujerumani Ujerumani Bendera ya Hispania Hispania Bendera ya Italia Italy
18. 2012-2016 Bendera ya Ujerumani Ujerumani Slovenia Bendera ya Hispania Hispania
19. 2012-2016 Bulgaria Bendera ya Ujerumani Ujerumani Bendera ya Ucheki Czech Republic
Bendera ya Poland Poland
20. 2016-2019 Bendera ya Ujerumani Ujerumani Bendera ya Urusi Urusi Bendera ya Hispania Hispania
21. 2020-2023 Bendera ya Ujerumani Ujerumani Luxemburg Marekani

Tanbihi

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Sataranji kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.