Nenda kwa yaliyomo

Lango:Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lango:Africa)

Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia

hariri  fuatilia  

Lango la Afrika

Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika.

Neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Roma ya Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile. Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini kwa Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).

hariri  fuatilia  

Nchi za Afrika

hariri  fuatilia  

Jamii

hariri  fuatilia  

Wasifu Uliochaguliwa

Desmond Tutu, Askofu mkuu Emeritus wa Cape Town

Desmond Mpilo Tutu (alizaliwa tarehe 7 Oktoba, mwaka 1931) ni Askofu mkuu wa Kanisa Anglikana nchini Afrika Kusini. Ilivyofika mwaka wa 1984 alipokea Tuzo ya Nobel ya Amani.

Maandiko : Crying in the Wilderness, 1982 ; Hope and Suffering: Sermons and Speeches, 1983 ; The Words of Desmond Tutu, 1989 ; The Rainbow People of God: The Making of a Peaceful Revolution, 1994 ; Worshipping Church in Africa, 1995 ; The Essential Desmond Tutu, 1997 ; No Future without Forgiveness, 1999 ; An African Prayerbook, 2000 ; God Has a Dream: A Vision of Hope for Our Time, 2004.

hariri  fuatilia  

Makala iliyochaguliwa

Jimbo Katoliki la Zanzibar (kwa Kilatini Dioecesis Zanzibarensis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, likienea katika visiwa vya Unguja na Pemba vya Tanzania visiwani, jumla kilometa mraba 2,332. Makao makuu yake ni katika mji wa Zanzibar na linahusiana na Jimbo kuu la Dar-es-Salaam. Kanisa kuu limewekwa wakfu kwa heshima ya Mtakatifu Yosefu. Askofu wa jimbo ni Augustine Ndeliakyama Shao, C.S.Sp. Jimbo liliundwa rasmi tarehe 28 Machi 1980 baada ya kujitegemea tangu 12 Desemba 1964 kama Apostolic Administration. Hata hivyo historia ni ndefu zaidi, kwa kuwa tangu mwaka 1860 Zanzibar ilikuwa makao makuu ya Apostolic Vicariate. Waumini ni 9.900 kati ya wakazi 990.900 (sawa na 1%), wengi wao wakiwa Waislamu. Mapadri ni 19, ambao kati yao 15 ni wanajimbo na 4 ni watawa. Hivyo kwa wastani kila mmoja anahudumia waumini 521 katika parokia 7. Mabruda jimboni ni 5, na masista 48.


hariri  fuatilia  

Picha Iliyochaguliwa


Kumbukumbu ya Kwame Nkrumah, Ghana.
(kupata bango)


hariri  fuatilia  

Je, wajua...?

...kwamba Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Eneo kuu na muhimukatika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikanandani ya hifadhi hii.

hariri  fuatilia  

Masharika ya Wikimedia