Bongiwe Dhlomo-Mautloa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bongiwe au Bongi Dhlomo-Mautloa (amezaliwa Vryheid, KwaZulu-Natal, 1956) ni raia wa Afrika ya Kusini mwenye asili ya Kizulu na hujishughulisha katika uchapishaji na usimamizi wa kazi za sanaa. Pia ni mwanaharakati. [1][2][3][4]

Amesoma shule ya mtakatifu Chad iliyopo Ladysmith, KwaZulu-Natal, na shule ya seminari ya Inanda. Alijifunza uchapishaji akiwa "Rorke's Drift Art and Craft Centre" ambapo alipata stashahada ya sanaa.[1]

Alifanya kazi katika kituo cha Sanaa cha African Art Centre huko Durban (mwaka 1980- 1983) kisha kufanya kazi katika jumba la maonyesho ya Sanaa la Grassroots katika mji huo huo wa Durban. Kabla ya kuhamia jiji la Johannesburg, alisimamia maonyesho katika jumba la maonyesho la Fub ana Goodman. [1]

Alikuwa mwanzilishi na mratibu wa mradi wa kituo cha Sanaa cha Alexandra, Gauteng iliyopo Johannesburg. Alikuwa msimamizi wa mradi wa maendeleo ya Johannesburg yam waka 1995 lililopewa jina la Africus. Pia alikuwa msimamizi wa tukio la mwaka 1997 lililotambulika kama Trade Routes: History and Geography.[2]

Alisema ya kuwa, maandamano ya Soweto ya mwaka 1976 akiwa na umri wa miaka 20, yalimfanya ajihusishe na siasa[4] na machapisho yake yakawa ya kisiasa mda wote ikielezea tukio hilo la kihistoria. [2] Kazi yake ilionekana katika jarida la "Staffrider".[2] Ameolewa na msanii wa maonyesho aitwayo Kagiso Patrick Mautloa [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Bongiwe (Bongi) Dhlomo-Mautloa". www.sahistory.org.za. South African History Online. Iliwekwa mnamo 31 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 Koloane, David (21 Machi 2000). "Dhlomo-Mautloa, Bongiwe". Oxford Art Online. doi:10.1093/gao/9781884446054.article.T096572.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Bongiwe Dhlomo-Mautloa". Asai. Africa South Art Initiative. Iliwekwa mnamo 31 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 Arnold, Marion (1 Januari 2011). "Cutting anti-apartheid images: Bongiwe Dhlomo's activist linocut prints". Katika Hoskins, S. (mhr.). IMPACT 6 Multi-disciplinary Printmaking Conference Proceedings. Impact Press. ku. 131–136. Iliwekwa mnamo 31 Januari 2021.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bongiwe Dhlomo-Mautloa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.