Kisukari (ugonjwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ueneaji wa kisukari mwaka 2014

Kisukari au bolisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini.

Dalili za kisukari ni

  • kukojoa kupita kiasi cha kawaida
  • kiu kubwa
  • kuona vibaya na matatizo ya macho hadi kuwa kipofu
  • kuchoka haraka
  • vidonda vinavyopoa polepole mno, hasa kwenye miguu, hadi kupotewa na viungo

Watu wachache huzaliwa na uhaba wa insulini. Walio wengi wana udhaifu fulani unaokuwa hatari kutokana na aina za vyakula na maisha ya kila siku. Kutumia sukari nyingi pamoja na mafuta mengi katika chakula na vinywaji, kukosa mazoezi ya mwili (kwa watu wenye kazi ofisini), kunywa pombe nyingi na kuvuta sigara huongeza hatari ya kushika kisukari kuanzia baada ya miaka ya ujana.

Ugonjwa wa kisukari husababishwa na kongosho (kwa Kiingereza "pancreas") kutoweza kutoa kiwango cha insulini mwilini kinachofaa. Pia yaweza kuwa mwili haufanyi kama unavyotarajiwa kufanya insulini ikifika sehemu ile ya mwili.

Kuna aina tatu za bolisukari:

  • Moja ni wakati kongosho imeshindwa kutengeneza insulini kiwango kizuri cha kudhibiti sukari mwilini
  • Aina ya pili ni wakati mwili unakataa kudhibiti sukari hata insulini ikitengenezwa na kongosho
  • Aina ya tatu ni bolisukari ambayo huathiri wanawake wajawazito ambao hupata kwamba kiwango cha sukari miilini mwao kimekwenda juu hata kama hawana historia ya aina hii.

Takwimu zadhihirisha kwamba mwaka 2015, watu milioni 415 duniani kote walikuwa na bolisukari[1]. Kisukari aina ya 2, yaani miili yao ilikataa kudhibiti sukari hata baada ya kongosho kutoa insulini, ilichangia asilimia tisini[2][3]. Hao ni asilimia 8.3 za watu wazima wote[3], wakiwemo wanaume na wanawake kwa uwiano sawa[4]. Mwelekeo ni wa kuongezeka zaidi na zaidi.[5]

Kisukari kinazidisha hatari ya kufa mapema walau mara mbili. Katika miaka 2012-2015, watu milioni 1.5 hadi 5.0 walifariki kila mwaka kutokana na kisukari.[1]

Hasara ya kiuchumi mwaka 2014 ilikadiriwa kuwa dola bilioni 612.[6]

Maelezo ya kisukari kwa njia ya video.

Kinga na tiba[hariri | hariri chanzo]

Unapotaka kujikinga na bolisukari, inafaa ule lishe bora, ufanye mazoezi, udhibiti uzani wako na usitumie sigara wala pombe.

Walio na shida ya kisukari wafaa kudhibiti shinikizo la damu pamoja na kuangalia miguu yao vizuri. Kuna viatu maalumu za kuvalia kwa walio na bolisukari.

Kwa walio na bolisukari aina ya kwanza, tiba ni kupokea sindano za insulini. Walio na aina ya pili ya bolisukari waweza kutibiwa kwa insulini au hata dawa nyingine. Wanawake walio na aina ya tatu ya bolisukari hupata kwamba bolisukari yao yaisha pindi tu wanapozaa.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Update 2015". ID F. International Diabetes Federation. uk. 13. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 21 Machi 2016. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Williams textbook of endocrinology (toleo la 12th). Elsevier/Saunders. 2011. ku. 1371–1435. ISBN 978-1-4377-0324-5.
  3. 3.0 3.1 Shi, Yuankai; Hu, Frank B (7 Juni 2014). "The global implications of diabetes and cancer". The Lancet. 383 (9933): 1947–48. doi:10.1016/S0140-6736(14)60886-2. PMID 24910221.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Vos T, Flaxman AD, Naghavi M, Lozano R, Michaud C, Ezzati M, Shibuya K, Salomon JA, Abdalla S, Aboyans V, na wenz. (15 Desemba 2012). "Years lived with disability (YLDs) for 1160 sequelae of 289 diseases and injuries 1990–2010: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2010". Lancet. 380 (9859): 2163–96. doi:10.1016/S0140-6736(12)61729-2. PMID 23245607.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Annual Report 2014" (PDF). IDF. International Diabetes Federation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 17 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 13 Julai 2016. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. IDF DIABETES ATLAS (PDF) (toleo la 6th). International Diabetes Federation. 2013. uk. 7. ISBN 2930229853. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 9 Juni 2014. {{cite book}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisukari (ugonjwa) kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.