Kolumba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtume wa Wapikti.

Kolumba (anajulikana pia kama Colum Cille, Colm Cille, Calum Cille, Colum Keeilley, Kolban na Kolbjørn, maana yake "Njiwa wa Kanisa"; 7 Desemba 5219 Juni 597) alikuwa mmonaki padri mmisionari kutoka Ireland aliyeeneza Ukristo kati ya Wapikti wa Uskoti.

Baada ya kupata malezi ya kitawa, alianzisha monasteri kadhaa maarufu kwa nidhamu na elimu, kwanza kwao, halafu katika kisiwa cha Iona (Uskoti) alipofariki mbele ya altare akiwa anamngojea Bwana[1].

Anahesabiwa kati ya Mitume kumi na wawili wa Ireland.

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe ya kifo chake, 9 Juni[2].

Sala yake[hariri | hariri chanzo]

Peke yangu, pasipo yeyote ila wewe, Mungu wangu, nasafiri katika njia yangu.

Niogope nini, ukiwa karibu nami, mtawala usiku na mchana?

Katika mkono wako niko salama kuliko kama ningezungukwa na jeshi la kunilinda.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Adomnán (c. 700), Reeves, William (mhr.), Life of Saint Columba, Founder of Hy., Edinburgh: Edmonston and Douglas (ilichapishwa mnamo 1874), iliwekwa mnamo 2008-09-14
  • Tranter, Nigel G. (1987), Historical novels by Nigel Tranter set before 1286, Hodder & Stoughton, ISBN 0-340-40699-2, iliwekwa mnamo 2008-09-14
  • Magnusson (1990), The Cambridge Biographical Dictionary, Cambridge University Press, ISBN 0-521-39518-6, iliwekwa mnamo 2008-09-14
  • Lewis, James (2007), Paths of Exile: Narratives of St. Columba and the Praxis of Iona, Cloverdale Corporation, ISBN 1-929569-24-6, iliwekwa mnamo 2008-09-14
  • Campbell, George F (2006), The First and Lost Iona, Glasgow: Candlemas Hill Publishing, ISBN 1-873586-13-2, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-14, iliwekwa mnamo 2012-09-08 {{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.