Valeri wa Zaragoza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa ukutani uliofanywa na msanii Francisco de Goya.

Valeri wa Zaragoza (alifariki 315 hivi) alikuwa askofu wa jimbo la Zaragoza, Hispania kuanzia mwaka 290 hadi kifodini chake[1].

Inasemekana alikuwa na shida katika kusema, hivyo alimtumia shemasi wake Vinsent kutoa ujumbe wake[2].

Wakati wa dhuluma ya Kaisari Dioklesian, Vinsent aliteswa vikali sana, akafa kwa ajili ya dini yake huko Valencia mwaka 304, kumbe askofu wake alipelekwa uhamishoni huko Enet, karibu na Barbastro[1]. Hata hivyo aliweza kushiriki mtaguso wa Elvira (306 hivi).[3].

Heshima ya watu kwake kama mtakatifu ni ya zamani sana.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Januari[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Amadó, Ramón Ruiz. "Saragossa." The Catholic Encyclopedia. Vol. 13. New York: Robert Appleton Company, 1912. 11 Feb. 2015
  2. ""St. Vincent of Saragossa, Deacon, first Martyr of Spain", St. Vincent Cathedral, Bedford, Texas". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-08. Iliwekwa mnamo 2020-04-19.
  3. Hefele, Karl Joseph von. A History of the Councils of the Church, from the Original Documents, Vol. 1, T. & T. Clark, 1883
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.