Nenda kwa yaliyomo

Agata Yi Kannan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Agata Yi Kannan (1814 - Sai-Nam-Hte, 20 Septemba 1846) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 17911888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.

Mjane huyo na wafiadini wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[1]

Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba[2].

Walionyongwa katika magereza mbalimbali siku moja naye ni: Laurenti Han Ihyong, Petro Nam Kyongmun, Suzana U Surim, Yosefu Im Chipek, Teresa Kim Imi na Katerina Chong Choryom[3].

Mazingira[hariri | hariri chanzo]

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu katika rasi ya Korea, nchi ya Kikonfusyo, kwa juhudi na ari za wananchi walei[4].

Mwaka 1836 Korea ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society) ambao walilisha na kuthibitisha imani kwa kutangaza Neno la Mungu na kuadhimisha sakramenti.

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Korea and the church of martyrs". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-07.
  2. Martyrologium Romanum
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/70880
  4. Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.