Nenda kwa yaliyomo

Internet Archive

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makao makuu ya Internet Archive huko San Fransisco.

Internet Archive ni shirika lisilotafuta faida linalojenga kumbukumbu ya kidijiti kwenye intaneti inayopatikana kwa kila mtu bila malipo.

Makao makuu ya shirika yapo San Francisco, Kalifornia (Marekani).

Lilianzishwa mwaka 1996 na Brewster Kahle kwa shabaha ya kutunza yaliyomo ya intaneti kwa kuhifadhi picha za tovuti nyingi. Kwa hiyo inawezekana kuangalia picha za tovuti ambazo zimeshabadilishwa tena mara kadhaa.

Tangu mwaka 1999 hifadhi nyingine zimeongezwa. Sasa kuna vitengo vya video, filamu, picha na vitabu.

Kitengo maalumu cha IA ni maktaba ya "Open Library". Vitabu visivyo tena na hakimiliki vinapigwa picha kila ukurasa kwa njia ya scanner na kuwekwa kwenye intaneti katika fomati mbalimbali.

Mashine ya scanner inayopiga picha za kurasa za vitabu

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: