Nenda kwa yaliyomo

Juma Hamad Omar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Juma Hamad Omar ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CUF. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Ole kwa miaka 20152020. [1]

Juma Omar alipata elimu yake ya msingi Skuli ya msingi Ngambwa (1960-1968) baadae kujiunga na elimu ya sekondari Fidel Castro (1969-1972) baadae elimu ya sekondari ya juu Lumumba (1973-1974).

Juma Omar alipata shahada yake ya mwanzo ya ualimu akibobea katika somo la fizikia chuo kikuu cha Dar es Salaam (1975-1978) na baadae kujiunga na chuo kikuu cha Reading (1980-1981) na kuchukua shahada ya uzamivu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania Archived 25 Januari 2020 at the Wayback Machine., iliangaliwa Mei 2017