Mafuta ya Mbarika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makokwa ya mbarika
Chupa ya mafuta ya mbarika

Mafuta ya Mbarika (pia yajulikana kama Mafuta ya Mbono) ni mafuta ya mboga yaliyoshindiliwa kutoka kwenye makokwa ya mbarika[1]. Ni kiowevu kisicho na rangi au cha rangi ya njano chenye ladha tofauti na harufu.

Yanajumuisha mchanganyiko wa triglycerides ambapo karibu 90% ya asidi ya mafuta ni ricinoleates [2]. Asidi ya rinoleic na linoleic ni sehemu nyingine muhimu.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Kila mwaka, takribani tani 270,000-360,000 za mafuta ya mbarika hutolewa kwa matumizi mbalimbali. [3] Kwa kawaida hutumiwa kama nyongeza katika vyakula, dawa, na bidhaa za utunzaji wa ngozi, na vilevile mafuta ya viwandani na mafuta ya dizeli.

Katika Misri ya kale, watu walichoma mafuta hayo katika taa, waliyatumia kama dawa ya asili ya kutibu magonjwa kama kuwasha kwa macho, na hata waliyachukua ili kuchochea uchungu wakati wa ujauzito.[4]

Muundo wa sehemu kuu ya mafuta ya mbarika : triester ya glycerol na asidi ya ricinoleic.

Mafuta ya mbarika yametumiwa kwa mdomo ili kupunguza kuvimbiwa au kutoa matumbo kabla ya upasuaji wa matumbo. [5]

Yanaweza kusaidia kupunguza kuvimbiwa na magonjwa ya ngozi na inaweza hata kutumika kama moisturizer asili ya ngozi na matibabu ya meno bandia.

Mafuta hayo yamekuwa yakitumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali [6] na kusaidia mfumo wa kingamaradhi.

Ingawa watu wengi hutumia mafuta hayo kama matibabu ya nywele kavu au nyembamba, hakuna ushahidi kwamba yanafaa kwa kuboresha afya ya nywele au kuchochea ukuaji wa nywele yanapotumiwa peke yake.

Mafuta ya Mbarika ni matibabu maarufu ya asili kwa hali ya kawaida kama vile kuvimbiwa. Mara nyingi unaweza kuyapata kati ya bidhaa za uzuri wa asili.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Faida za mafuta ya mbarika yaani castor oil – Taifa Leo" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-09-03.
  2. Thomas, Alfred (2005). "Fats and Fatty Oils". Ullmann's Encyclopedia of Industrial Chemistry. Weinheim: Wiley-VCH. doi:10.1002/14356007.a10_173. ISBN 978-3527306732.
  3. Mutlu, H; Meier, MAR (Januari 2010). "Castor oil as a renewable resource for the chemical industry". European Journal of Lipid Science and Technology. 112 (1): 10–30. doi:10.1002/ejlt.200900138.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Nathan, Alan (2010). Non-prescription Medicines (kwa Kiingereza). Pharmaceutical Press. ISBN 978-0-85369-886-9.
  5. "Castor oil". Drugs.com. 3 Oktoba 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Aprili 2023. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "How to Use Castor Oil to Detox the Liver and Kidneys - Article Zone" (kwa American English). 2023-09-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-09-03. Iliwekwa mnamo 2023-09-03.