Pasienti wa Lyon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pasienti wa Lyon (alifariki 480 hivi) alikuwa askofu mkuu wa mji huo, leo nchini Ufaransa [1] kuanzia mwaka 450 hivi.

Akisukumwa na upendo, aligawa bure ngano kwa miji ya kando ya mito Rhone na Saone hasa njaa ilipoenea nchini naye akatumia mali zake zote kulisha watu wa jimbo lake na nje yake pia; akajitosa katika utume wa kurudisha wazushi na kuhudumia wenye shida mbalimbali [2][3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Septemba[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.