Yohane Gabrieli Perboyre

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Yohane Gabrieli akiwa katika mavazi ya Kichina.

Yohane Gabrieli Perboyre, C.M. (Montgesty, Lot, 6 Januari 1802Wuchang, Hubei, 11 Septemba 1840) alikuwa padri wa shirika la Vinsenti kutoka Ufaransa aliyefanya umisionari nchini China.

Katika kuhubiri Injili alijilinganisha na desturi za wananchi, lakini dhuluma ilipolipuka aliteswa kwa namna mbalimbali wakati wa kufungwa kwa muda mrefu akauawa huko msalabani kwa ajili ya imani yake ya Kikristo[1].

Alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 10 Novemba 1889, halafu mtakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 2 Juni 1996[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/76475
  2. Miller, Charles Edward (2004). Mass on Sunday: And Other Ways of Being Catholic. Paulist Press. ku. 45–46. ISBN 0-8091-4237-6.
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.